HabariMilele FmSwahili

Watu 3 wauwawa na 5 wajeruhiwa kwa kupigwa risasi eneo la Manyatta, Marsabit

Watu watatu wameuawa huku wengine tano wakijeruhiwa baada ya kupigwa risasi eneo la Manyatta Konso kaunti ya Marsabit.  Kulingana na kamanda wa polisi eneo hilo Steve Oloo, watu nne walivamia kijiji hicho na kuwamiminia risasi wakaazi usiku wa kuamkia leo. Oloo amesema waliouawa ni wanawake wawili na mtoto mmoja. Aidha wakaazi wanadai kisa hicho kimechochewa na matamshi ya wanasiasa kwenye kaunti hiyo.  Hapo jana watu wawili waliuawa eneo la Milima Shaba.  Idadi ya waliopoteza maisha yao katika kipindi cha majuma mawili yaliyopita imefikia watu 18

Show More

Related Articles