HabariMilele FmSwahili

Watu 2 wafariki katika ajali kwenye barabara ya Nandi Hills – Chemelil

Watu wawili wameaga dunia na wengine kumi na sita kujeruhiwa  baada ya gari aina ya Nissan walimokuwa wakisafiria kupata ajali katika barabara ya Nandi Hills kuelekea Chemelil.

Abiria hao walikuwa wakitoka kwenye sherehe za kufuzu kwa makurutu wa jeshi mjini Eldoret pale dereva alipokosa mwelekeo alipohepa kumgonga mhudumu wa bodaboda na kuishia kubingiria mara kadhaa.

Majeruhi wanapokea matibabu katika hospitali ya  Nandi Hills na ile ya rufaa ya Eldoret huku mili ya wafu ikipelekwa katika chumba cha wafu cha Kapsabet.

Show More

Related Articles