HabariMilele FmSwahili

Watu 16 kufikishwa mahakamani baada ya kunaswa na ERC kwa kuuza mafuta kinyume na sheria Nairobi

Watu 16 wanatarajiwa mahakamani baada ya kunaaswa kwenye msako ulioendeshwa na  tume ya kudhibiti kawi  ERC kwa kuuza mafuta kinyume na sheria hapa Nairobi. Mkurugenzi wa ERC Pavel Oimeke anasema wametambua vituo 5 huku vituo vingine 100 vikifungwa katika miji ya Eldoret na Kisumu. Anasema biashara hiyo ni hatari kwa mazingira wenyeji  na kwa magari  yanayowekwa mafuta hayo. Lita 8000 za  mafuta aina ya petroli zilipatikana wakati wa msako huo katika maeneo ya  Industrial Area mtaani South B.

Show More

Related Articles