HabariMilele FmSwahili

Watu 15 walazwa katika kituo cha afya baada ya mkurupuko wa ugonjwa wa Malaria kuripotiwa kaunti ya Baringo

Watu kumi na tano wamelazwa katika kituo cha afya cha Kapau kufuatia mkurupuko wa ugonjwa wa Malaria ulioripotiwa katika wadi ya Tirioko kaunti ya Baringo.

Afisa mkuu wa afya eneo hilo Gideon Torome anasema madaktari sita zaidi wametumwa katika eneo zima la Tiaty kuthamini hali.

Torome anasema miongoni mwa vijiji vilivyoathirika ni Okapau, Korelach, Lokis, Chesawach, Ng’aina, Chesotim, Akoret, Kong’or, Krese na Kulol

Show More

Related Articles