HabariMilele FmSwahili

Watu 10 waangamia baada ya basi kugonga trela eneo la Tula kaunti ya Garissa

Takribani watu 10 wameangamia baada ya basi kugonga trela katika eneo la Tula kwenye bara bara ya Garissa kuelekea Nairobi. Kulingana na shirika la msalaba mwekundu watu 14 wamekimbizwa katika hospitali kuu ya Garisa wakiwa na majeraha mabaya. Shirika hilo limedhibitisha kuwa basi la Nasib sacco lililokuwa likitoka Nairobi kuelekea garisa liligonga trela lililokuwa limesimama.

Show More

Related Articles