HabariMilele FmSwahili

Washukiwa 6 wa mauaji ya mwanaharakati Carol Mwatha kuzuiliwa kwa siku 14

Mahakama imeagiza kuzuliwa a siku 14 washukiwa  6 wanaohusishwa na mauaji ya mtetezi wa haki za kibinadamu Carol Mwatha. Mahakama inasema muda huo utatumika na polisi kubaini mchango wa 6 hao katika mauaji ya Mwatha. Uchunguzi wa awali wa polisi unasema mwatha alifariki alipokuwa wakijaribu kuavya mimba ya miezi 5 katika kliniki moja mtaani Dandora.

Yakijiri hayo familia ya mwanaharakati Caro Mwatha imelalamikia hatua ya kuhairishwa upasuaji wa mwili wa ke hadi Jumatatu. Babake mwendazake amekosa hatua hiyo akisema huenda kuna njama ya kuficha ukweli kuhusu kifo cha Caroline.

Akiunga mkono msimamo huo, mumewe marehemu amepinga madai kwamba mkewe alifariki akiaavya mimba.

Wanaharakati sasa wanatishia kuandamana iwapo mwili wa Caroline hautafanyiwa upasuaji leo

Show More

Related Articles