HabariMilele FmSwahili

Washukiwa 4 wa shambulizi la kigaidi katika chuo kikuu cha Garissa kufikishwa mahakama leo

Washukiwa wanne katika kesi kuhusu shambulizi ya kigaidi dhidi ya chuo kikuu cha Garissa mwaka wa 2015 watabaini hatma yao leo. Hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani  Francis Andayi, anatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya Mohamed Abikar, Hassan Edin Hassan, Sahal Diriy na Mtanzania Rashid Charles Mberesero. Wanne hao wanatuhumiwa kupanga njama ya mauaji ya wanafunzi 144, walinzi wanne na wafanyikazi wengine 2 wa chuo hicho. Inakisiwa huenda 4 hao wakahukumiwa maisha gerezani.

Show More

Related Articles