HabariMilele FmSwahili

Washukiwa 3 wa sakata ya Rio waachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 1

Washukiwa watatu wa sakata ya Rio wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi millioni 1 baada ya kukana mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi. Aliyekuwa katibu wa michezo Richard Ekai, msimamizi wa zamani wa michezo Rio Stephen Soi na katibu mkuu wa shirikisho la olimpiki Francis Kinyili maarufu kama FK Paul wamekanusha mashtaka ya ubadhirifu wa shilingi milioni 55. Jaji Douglas Ogoti aidha amewapa hadi alhamisi wiki hii ,aliyekuwa waziri wa michezo Hassan Wario pamoja na mwenyekiti wa zamani wa kamati ya olimpiki nchini Kipchoge Keino kuijiwasilisha kwa idara ya jinai DCI la usivyo kibali cha kukamatwa kwao kitolewe.

Show More

Related Articles