HabariMilele FmSwahili

Wahudumu wa texi za kidigitali kukutana na waziri Matiangi kujadili usalama wao leo

Wahudumu wa texi wa kidigitali wanatarajiwa leo hii kukutana na waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiangi kujadili kuhusu usalama wao. Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Ryan Kanyadong anasema wahudumu hao wanapendekeza sera za usalama katika kaunti ya Nairobi kufanyiwa marekebisho kurahisisha ufuatialiaji wa visa vya ukosefu wa usalama. Akirejelea mgomo wa wahudumu hao,Kanyadong anashikilia utafika kikomo punde tu mwafaka utakapoafikiwa.

Show More

Related Articles