HabariMilele FmSwahili

Wahudumu wa teksi za mitandao waanza mgomo wao rasmi

Wahudumu wa teksi za mitandao wameanza mgomo wao rasmi. Wanalalamikia mazingira duni ya kufanyia kazi,mishahara duni na kudhalilishwa na mwajiri wao. Wahudumu hao wa teksi za Bolt na Uber wanasema juhudi zao kutaka mazungumzo na mwajiri wao zimeambulia patupu na njia ya kipekee kushinikiza haki ni kususia kazi. Wakiongozwa na Ryayan Kanyandong,wanasema hawatarejea kazini hadi kilio chao kisikizwe. Wanasema wanachotaka ni wateja kulipishwa ada za usafiri kulingana na aina ya gari,wapewe usalama wa kutosha hasa nyakati za usiku na pia kuwepo sheria madhubuti kudhibiti biashara hizo.

Show More

Related Articles