HabariMilele FmSwahili

Wafanyikazi 18 wa kampuni ya Kenya Power wafutwa kazi

Wafanyikazi 18 wa kampuni ya umeme ya Kenya Power wamefutwa kazi kwa kujihusisha na ufisadi huku mwengine mmoja aliyesimamishwa kazi akipatikana bila hatia. Mkurugenzi wa Kenya Power Ken Tarus anasema uamuzi huo umeafikiwa baada ya ushahidi kuonyesha wahusika walitoa kandarasi za mabilioni ya pesa kinyume na sheria. Hata hivyo Tarus anasema hakuna pesa za kampuni hiyo zimepotea huku akiwahakikishia wakenya kuwa wanafanya kila wawezalo kuimarisha huduma zao

Show More

Related Articles