HabariMilele FmSwahili

Wafanyibiashara wakadiria hasara baada ya vibanda vyao kubomolewa eneo la Bandani, Kisumu

Zaidi ya wafanyabiashara 300 eneo la Bandani,karibu na uwanja wa ndege wa Kisumu wanakadiria hasara baada ya serikali ya kaunti kubomoa vibanda vyao.

Ni miongoni mwa misururu ya ubomozi unaoendeshwa ili kufanikisha upanuzi wa poti ya Kisumu sawa na uboreshwaji wa safari za reli.

Hata hivyo wafanyabiashara walioathirika wakiongozwa na Richard Osanyo wanaisuta serikali ya kaunti hiyo kwa kutowapa notisi ya mapema.

Sasa wanamtaka gavana prof Peter Anyang Nyongo kuingilia kati kwa haraka kuhakikisha wamepata sehemu nyingine ya kuendesha biashara zao.

Show More

Related Articles