HabariMilele FmSwahili

Wafanyibiashara 2 waliokamatwa na mchele ulioharibika kuzuiliwa kwa siku 10

Mahakama imeagiza kuzuiliwa kwa wafanyibiashara wawili  kwa muda wa siku 10 wafanyibiashara waliopatikana na mchele  usiofaa  katika mtaa wa Kariobangi  hapa Nairobi.Hakimu Paul Mayoya amewapa polisi ruhusa ya kuendelea kuwazuilia Mbugua Kariuki, na Jeremiah Kuria kimani katika kituo cha polisi cha Parklands. Wawili hao walifumaniwa wakipakia mchele ambao haukuwa salama kwa matumizi ya binadamu kwenye gunia tayari  kuuza. Mchele huo ulikuwa ukitolewa kwenye mifuko yenye jina Amar na day to day na kuwekwa kwenye ile  jina Red Rose na Pick Cock

Show More

Related Articles