HabariMilele FmSwahili

Wabunge wataka kujumuishwa kwenye bima ya afya wake wao wengi

Wabunge kwa mara nyingine wametaka kujumuishwa kwenye bima ya afya wake wao wengi. Wabunge hao ambao hawakutaka majina yao kutajwa wanadai kuwa ni kinyume na katiba kuwaacha nje ya bima hiyo wake zao zaidi. Pia wamepinga huduma wanazopokea sasa za bima kutoka kampuni ya humu nchini wakizitaja kutotosheleza mahitaji yao na kuwa mara nyingi wamelazimika kugharamia huduma za afya. Shinikizo hili linajiri mwaka mmoja baada ya mbunge wa Budalangi Raphael Wanjala kuapa kushinikiza wake zaidi wa wabunge kufaidika na bima hiyo.

Ilivyo sasa wabunge wana bima ya afya ya hadi shilingi milioni 10 kwa wanaolazwa, shilingi laki 1 50 kwa huduma ya kujifungua kina mama na shilingi elfu 75 kwa huduma za matibabu ya mano. Kwa sasa bima hiyo inawafaidi mbunge mke mmoja na watoto wake wanne wenye miaka 25.

Show More

Related Articles