HabariMilele FmSwahili

Viongozi mbalimbali wazidi kuomboleza kifo cha mwanamuziki John De Mathew

Viongozi mbalimbali hasaa kutoka eneo la mlima Kenya wanazidi kutuma risala za rambi rambi kwa jamaa ndugu na marafiki wa mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za benga za Kikuyu John Nganga maarufu John De Mathew.

Mbunge wa Runyenjes Cecily Mbarire anasema kifo cha De Mathew ni pigo kubwa kwa sekta ya usanii.

Amempongeza kwa ubunifu katika utunzi wa nyimbo zake hali iliyomfanya kupendwa na wengi hasaa kutoka jamii ya Agikuyu.

De Mathew alipoteza maisha yake katika ajali ya barabarani usiku wa kuamkia leo katika eneo la Blue Post kwenye barabara kuu ya Thika

Show More

Related Articles