HabariMilele FmSwahili

Vikao vya umma kuwasilisha ushahidi kuhusu mauaji ya mtoto Pendo kuendelea Kisumu

Vikao vya umma kuwasilisha ushahidi kuhusiana na mauaji ya mtoto Pendo vinaendelea asubuhi hii mjini Kisumu. Mtoto huyo aliarifiwa kupigwa na kuuwawa na maafisa wa polisi waliokuwa wakikabili ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana. Aliyekuwa mkurugenzi wa mashitaka ya umma Keriako Tobiko aliagiza kufanyika vikao hivyo maafisa kadhaa wakuu wa polisi waliohudhumu Kisumu wakati huo wakituhumiwa kuhusiana na mauaji hayo. Upande wa mashitaka unasema unanuia kuwaita mashaidi 21 mbele ya hakimu wa mahakama kuu ya Kisumu Beryl Omollo

Show More

Related Articles