HabariMilele FmSwahili

Vijana waandamana Nairobi kulalamikia ukosefu wa ajira

Vijana wasiokuwa na ajira wameandamana hapa Nairobi kulalamikia hali hii. Vijana hao waliovalia tisheti nyekundu kuashiria hatari wanasema ukosefu wa ajira nchini umefikia hali mbaya wakituhumu serikali kwa hali husika.

Waandamanaji hawa waliohusisha kundi la vijana waliofutwa kazi kutoka kampuni za wacheza kamari ambazo zilifungwa juma jana wanasema serikali ndio  ya kulaumiwa kwa kukosa kutoa mazingria bora ya kufanya kazi sawa na kukosa kutimziwa ahadi ya kubuniwa ajira kama ilivyoahidi serikali ya jubilee mwaka 2017 wakati wa uchaguzi.

 

Show More

Related Articles