HabariMichezoMilele Fm

Victor Wanyama asaka uraia wa Uingereza

Nahodha wa timu ya taifa ya soka Harambee Stars Victor Wanyama amesema ananuia kupata uraia wa taifa la Uingereza ili kumwezesha kuishi nchini humo atakapomaliza taaluma yake ya soka.

Katika mazungumzo ya kipekee na Uga wa Milele,Wanyama amesema hana njama fiche ya kuisaliti Kenya kisoka na kwamba bado angali na uzalendo.

“Mimi ni mkenya na nimechezea Kenya,hayo mambo mengi haya maana kwa sasa. Nia yangu ni kupata kibali cha kukaa Uingereza nitakapo maliza taaluma yangu ya soka. Si kwamba nabadilisha uraia,mimi bado mkenya,”ameeleza Wanyama.

Endapo atafaulu katika azimio lake,atakuwa mchezaji wa pili wa hivi punde kusaka uraia wa taifa lingine baada ya mlinda lango wa zamani wa Stars Arnold Origi kuhamia Norway 2017.

Mchanaji huyo hodari ameahidi kuweka juhudi zaidi ili kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kocha Mauricio Pochetino katika msimu mpya wa soka barani Uropa.

Tottenham imemsajili kiungu mfaransa Tanguy Ndombele kutoka klabu ya Lyon kwa pauni milioni 54,usajili ambao huwenda ukapunguza nafasi za Wanyama kusalia London na klabu hiyo iliyotinga fainali ya taji la klabu bingwa Ulaya msimu jana.

“Bado nina kandarasi na Spurs na narejea nikiwa na moyo kwa kupambana zaidi msimu unaokuja,” ameongeza Wanyama.

Wanyama 27,amefunga safari Jumapili usiku kuelekea Uchina ambako anatarajiwa kuungana wachezaji wenzake wa Tottenham wanaojifua kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu England.

Spurs itafungua kampeini mpya ya ligi ya Uingereza dhidi ya Aston Villa tarehe 10 Agosti.

Show More

Related Articles