HabariMilele FmSwahili

Upasuaji wa maiti ya Tob Cohen kufanyika kesho

Upasuaji wa mwili wa bwenyenye Tob Cohen umehairishwa hadi kesho.Upasuaji wa mwili huu utafanywa na wanapatholojia 3, yule wa serikali Johansen Odour, mwanapatholojia wa kibianfisi kutoka familia ya Cohen na mwingine kutoka familia ya mkewe Cohen, Sarah Wairimu. Mawakili wa pande husika pia watahusika katika shughuli hii. Philip Murgor ni wakili wa Sarah Wairimu,mkewe Tob Cohen na mmoja wa washukiwa wa mauaji haya.

Murgor anasema ameandikia mahakama kuu, afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma na idara ya jinai akitaka baadhi ya masharti yatimizwe kwenye uchunguzi wa kubaini ukweli kuhusu mauaji haya.

Mwili wa Cohen ulipatikana kwenye tangi la maji nyumbani kwake Ijumaa iliyopita mtaani Kitisuru viungani mwa jiji la Nairobi

Show More

Related Articles