HabariMilele FmSwahili

Uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa Gavana wa Nyeri Wahome Gakuru waanza upya

Mahakama ya Nyeri leo inaanzisha upya vikao vya kupokea ushahidi kuhusiana na kifo cha aliyekuwa gavana wa 3 Nyeri Wahome Gakuru. Zoezi hilo lililoanzishwa Januari mwaka huu lilisitishwa baada ya aliyekuwa hakimu Maisy Chesang aliyekuwa anasimamia shughuli hiyo kukamatwa kwa tuhuma za mauaji ya mumewe wakili Rober Chesang. Mmoja wa waliokuwa wasaidizi wa marehemu Gakuru  na ambaye alijeruhiwa kwenye ajali hiyio ameratibiwa kuelezea mahakama kilichojiri.

Show More

Related Articles