HabariMilele FmSwahili

Uchukuzi kutatizika katika barabara kuu ya Thika

Usafiri katika barabara kuu ya Thika unatarajiwa kutatizika kufuatia mpango wa mamlaka ya usimamizi wa barabara kuu mijini  KURA kufunga sehemu ya barabara hiyo eneo la Ruaraka  kuanzia leo.

KURA inalenga kufunga barabara hiyo kwa muda wa mwezi mmoja ili kutoa nafasi ya ukarabati wa kuipanua. Kufuatia hilo idara ya trafiki imetoa wito kwa  madereva kuzingatia  ipasavyo alama za trafiki zilizoezekwa katika sehemu mbalimbali za barabara hiyo.

Aidha umma umetakiwa kuridhia mabadiliko hayo kwani ukarabati unaoendeshwa unalenga kupunguza msongamano unaoshuhudiwa katika barabara hio mara kwa mara

Show More

Related Articles