HabariMilele FmSwahili

Uchaguzi mdogo eneo la Kibra kufanyika tarehe 7 mwezi November

Uchaguzi mdogo eneo bunge la Kibra utafanyika tarehe 7 mwezi Novemba. Tume ya uchaguzi na mipaka IEBC imetangaza tarehe hiyo na kutoa nafasi ya kuanza kwa mchakato wa kusaka kiti hicho kilichoachwa wazi kufuatia kifo cha Ken okoth.

IEBC imetoa tangazo hilo baada ya spika wa bunge la taifa Justine Muturi kutangaza kiti hicho kuwa wazi kwa mujibu wa sheria.

Tayari wagombea kadhaa wametangaza nia ya kupigania kiti hicho.

Show More

Related Articles