HabariMilele FmSwahili

Tume ya NCIC yataja kaunti 8 zilizo na visa vingi vya matamshi ya chuki

Tume ya uwiano wa kitaifa NCIC imetaja kaunti 8 kama zilizo na visa vingi vya utoaji wa matamshi ya chuki. Kaunti ambazo zimetajwa na tume hiyo ni pamoja na ile ya Kiambu, Kilifi, Uasin Gishu, Elgeyo Marakwet, Baringo, Nakuru, Nyeri na Kakamega. Afisa mkuu mtendaji wa NCIC Mohammed Hassan anasema taarifa zao zimekusanywa  kutoka kwa maafisa wa NCIC waliotumwa kaunti tofauti na vinasa sauti kukusanya data hizo.

Show More

Related Articles