HabariMilele FmSwahili

TSC yawafuta kazi walimu 36 kwa utovu wa nidhamu

Tume ya kuwajiri walimu nchini TSC imewafuta kazi walimu 36 kwa utovu wa nidhamu.  Afisa mkuu mtendaji Nancy Macharia anasema waalimu hao tayari wameondolewa kwenye sajili ya TSC.

Katika taarifa TSC inasema walimu hao walipatikana na hatia ya kushiriki kimapenzi na wanafunzi wao miongoni mwa makosa mengine.

Mwezi jana TSC iliwafuta kazi walimu 42 kwa kukosa kuhudhuria mafunzo ya  mtaala mpya wa CBC. Zaidi ya walimu 124 wamesimamishwa kazi kwa muda huku 30 kati yao wakiwa tayari wamekabidhiwa barua za onyo

Show More

Related Articles