HabariMilele FmSwahili

Trela la petroli laanguka na kutatiza shughuli za uchukuzi katika barabara ya Nakuru-Eldoret

Shughuli za uchukuzi zimetatizwa katika barabara kuu ya Nakuru kuelekea Eldoret eneo la Kamara Kuresoi Kaskazini baada ya trela la petroli kuanguka na mafuta kumwagika.

Polisi wamelazimika kutumia vitoa  machozi kuwatawanya raia walionuia kufyonza mafuta kutoka kwa lori hilo.

Dereva wa lori hilo alipoteza mwelekeo kabla ya kuangusha lori hilo.Polisi wamezingira eneo hilo kuzuia maafa.

Show More

Related Articles