HabariMilele FmSwahili

Tani kadhaa za mchele ulioharibika zanashwa eneo la Kariobangi South Nairobi

Makachero wa idara ya jinai hapa Nairobi wamefanikiwa kunasa tani kadhaa za mchele ulioharibika na ambao ulikuwa ukipakiwa upya kwa lengo la kuuzwa. Mkurugenzi wa DCI George Kinoti anasema makachero wake walivamia bohari moja eneo la Kariobangi South na kuwanasa watu wakipakia mchele huo wenye nembo za Amar na Day to Day kwenye mifuko mipya yenye nembo za Red ross na Peackock Parboiled Five Star. Kinoti anasema maafisa wa afya ya umma pia wamefika eneo hilo kwa ukaguzi wa kina kwani kuna vyakula  vingi vilivyo hifadhi kwenye bohari hilo.

Show More

Related Articles