HabariMilele FmSwahili

Spika Beatrice Elachi avamiwa katika majengo ya bunge la kaunti ya Nairobi

Kizazaa kinazidi kushuhudiwa ndani ya majengo ya bunge la kaunti ya Nairobi. Baadhi ya waakilishi wadi wakiongozwa na kiongozi wa wengi Abdi Guyo wakishikilia hawatamruhusi  spika wa bunge hilo Beatrice Elachi kutekeleza majukumu yake. Guyo na wenzake walivamia afisi za Elachi na kuzua taharuki pamoja na kuvunja mali afisini mwake hali iliowalazimu polisi kurusha vitoa machozi.

Purukushani hizi zikimtia hofu Bi Elachi ambaye sasa anadai maisha yake yamo hatarini.

hata hivyo mwakilishi wadi ya Ngara Chege Mwaura ambaye ni miongoni mwa wanaopinga Elachi wanadai mshikemshike huu utasalia kwani Elachi hafai kuwaongoza.

Show More

Related Articles