HabariMilele FmSwahili

Shughuli za kawaida zaendelea kushuhudiwa katikati mwa jiji la Nairobi

Shughuli za kawaida zimeendelea kushuhudiwa kati kati mwa jiji biashara nyingi zikifunguliwa. Hali hii inashuhudiwa licha ya agizo la kinara wa upinzani Raila Odinga kwa wafuasi wake kutoingia kazini leo. Kulingana na tuliozungumza nao, wito wa kinara huyo unalenga kulemaza uchumi wa taifa. Wakati uo huo kamanda wa polisi kaunti ya Nairobi Japhet Koome amewahakikishia wakazi hali ya kawaida imerejea hapa jijini. Ametoa hakikisho polisi wataendelea kutekeleza wajibu wao wa kulinda maisha na mali ya wakenya.

Show More

Related Articles