HabariMilele FmSwahili

SGR yaongeza siku za kununua tiketi ya usafiri kutoka 14 kuwa 30

Sasa unaweza kununua tiketi ya usafiri kutumia reli ya kisasa ya SGR kutoka Nairobi hadi Mombasa na kurudi siku 30 kabla ya kusafiri. Shirika la reli nchini linasema siku hizo zimeongezwa kutoka 14 ilivyokua awali hadi 30 kuwawezesha wakenya wengi kununua tiketi hizo kwa wakati unaofaa. Utekelezwaji wa mabadiliko hayo unaanza rasmi hi leo. Katika taarifa, KRC imewaahidi wakenya huduma bora kutumia usafiri wa SGR ambao ujenzi wake wa awamu ya pili kutoka Nairobi hadi Naivasha kuelekea malaba tayari umeanza

Show More

Related Articles