HabariMilele FmSwahili

Serikali yatenga bilioni 1.5 kuboresha miundo msingi katika shule za humu nchini

Serikali imeipa wizara ya elimu shilingi bilioni 1.5 kufanikisha ujenzi wa miundo msingi katika shule za humu nchini. Waziri wa elimu prof George Magoha anasema watahakikisha kila shule inayostahili kupokea mgao wake inaupokea ili kuinua viwango vya masomo kote nchini. Magoha aliyadokeza haya akiwa ziarani huko Kisii alikokwenda kushuhudia mafunzo ya mtaala mpya kwa walimu wa shule za msingi.

Magoha pia ametoa wito kwa wadau katika sekta ya elimu kuhakikisha mtaala mpya unaafikia kiwango kinachostahili katika wakati uliotengwa.

Show More

Related Articles