HabariMilele FmSwahili

Serikali yasitisha huduma za kulazwa wangonjwa kwenye hospitali ya rufaa ya Kerugoya

Serikali imesitisha huduma za kulazwa wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya Kerugoya kaunti ya Kirinyaga. Kufuatia hatua hii ni huduma za dharura pekee zitakazotolewa kwenye hospitali hiyo. Haya yanajiri kufuatia hali duni ya usafi inayoshuhudiwa kwenye hospitali hiyo kufuatia kufutwa kazi wafanyikazi 300.

Mapema leo gavana wa Kiriyanga Anne Waiguru sasa amedai mzozo unaoshuhudiwa kaunti yake unaibuliwa na maafisa wa afya wanaopinga kuondolewa wafanyakazi hewa kaunti hiyo. Katika mkao alioongoza mapema leo na jopo kazi aliloteuwa wikendi kushughulikia hali ya usafi hospitalini Kerogoya, Waiguru ameagiza jopo hilo kukagua hospitali zote kaunti hiyo katika muda wa siku 21 na kuandaa ripoti kuhusu jinsi ya kuiamrisha utoaji huduma. Kadhalika Waiguru amedhibitisha kwamba usafi umeanza kurejea hospialini Kerugoya.

Show More

Related Articles