MakalaMilele FmSwahili

Serikali yahakikishia wanaoishi na virusi vya HIV zipo dawa za kutosha

Serikali imewahakikishia wanaoishi na virusi vya  HIV kwamba zipo dawa za kutosha za kupunguza makali. Ni baada ya shughuli ya kuwasambazia dawa hizo kucheleweshwa.Katibu katika wizara ya afya Peter Tum anasema hali hiyo imetokana na ukaguzi wa kila miezi 3 kuangazia idadi ya dawa hizo nchini. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Tum hata hivyo anasema zipo dawa za kutosheleza mahitaji ya waathiriwa kwa miezi 15 ijayo.

Show More

Related Articles