HabariMilele FmSwahili

Serikali yaanza kuwafidia wamiliki wa ardhi Nkoroi kaunti ya Kajiado

Wamiliki ardhi katika eneo la Nkoroi kaunti ya Kajiado ambao ardhi zao zilitwaliwa kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa wataanza kulipwa fidia leo. Kulingana na mbunge wa Kajiado Kaskazini  Joseph Manje fidia hiyo italipwa katika awamu tatu ikianzia na wanaodai shilingi milioni 10 au kiasi cha chini. Wanaodai zaidi ya shilingi milioni 10 watalipwa katika awamu ya pili huku tume ya kukabili ufisadi ikitarajiwa kubaini kiasi watakacholipwa wale waliooorodheshwa katika awamu ya 3.

Haya yamebainika baada ya wakazi hao kukutana na maafisa wa tume ya kitaifa ya ardhi kuangazia hatma yao baada ya nyumba zao kubomolewa Ijumaa wiki jana ili kuruhusu ujenzi wa reli ya kisasa.

Show More

Related Articles