HabariMilele FmSwahili

KNBS :Sensa ya mwaka huu kugharimu wakenya shilingi bilioni 18.5

Itawagharimu wakenya bilioni 18.5 kufanikisha zoezi la sensa mwaka huu. Kwa mujibu wa shirika la kitaifa la Takwimu,zoezi hio litang’oa nanga tarehe 24 hadi tarehe 31 mwezi Agosti. Kufikia sasa wakenya 164,000 wameidhinishwa kuendesha shughuli hiyo muhimu. Hata hivyo ndani ya wiki 2 zijazo shirika hilo limeahidi kuchapisha rasmi   matangazo ya kutafuta watu zaidi wa kufanikisha shughuli hiyo. Hii ni kufuatia tetesi za kundi la watu linalodaiwa kuwatapeli wakenya kwa kuendesha matangazo hayo. Itakumbukwa awamu hii ya 8 ya zoezi la kuwahesabu wakenya inalenga kutoa takwimu ya wakenya wote ili kuiwezesha serikali kuweka kubuni   bajeti ya kutosha kuwahudumia.

Show More

Related Articles