HabariMilele FmSwahili

Sekta nyingi za biashara zaathirika kufuatia maandamano ya NASA

Sekta nyingi za biashara zimeathirika kufuatia maandamano ya kuibandua tume ya uchaguzi na mipaka IEBC. Muungano wa sekta ya binafsi nchini KEPSA unasema wafanyibiashara wanakadiara hasara kubwa kutokana na maandamano hayo. Wakizungumza baada ya kukutana na viongozi wa sekta mbalimbali, wakiongozwa na afisa mkuu mtendaji wa KEPSA Carol Kariuki wanasema maandamano haya yameibua taharuki nchini na kuwatia hofu zaidi wafanyobiashara.
Sekta ya matatu nayo inasema imenakili hasara ya asilimia 30 kufuatia hofu ya wamiliki kuyaweka magari yao barabarani kuhudumu. Mwenyekiti wa wamiliki matatu Simon Kimutai ameomba wanasiasa kutoendelea kuibua joto la kisiasa nchini.

Show More

Related Articles