HabariMilele FmSwahili

Sarah Wairimu aachiliwa kwa dhamana ya milioni 2

Mahakama ya Milimani memwachilia kwa dhamana ya shilingi milioni mbili pesa taslimu au bondi ya shilingi milioni nne ya wadhamini wa shilingi milioni mbili mkewe bwenyenye marehemu Tob Cohen Sarah Wairimu.

Jaji Stella Mutuku anasema upande wa mashtaka haujatoa sababu za kutosha kuendelea kumzuilia Sarah ambaye ni mshukiwa mkuu wa mauaji ya mumewe Tob Cohen.

Hata hivyo mahakama imewataka wazazi wake sawa na marafiki wake wawili kuwasilisha dhibitisho kuwa watampa makao baada ya kuzuiliwa kurejea kwake ili kuzuia kutatizwa kwa ushahidi.

Wakati uo huo imemtaka Saraha kutowasiliana na wanawe wawili miongoni mwa masharti mengine

Hata hivyo afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka inapania kukata rufaa dhidi ya uamzui wa mahakama kumpa dhamana Wairimu.Wakati uo huo mshukiwa wa pili katika mauaji hayo Peter Karanja amekana mashtaka ya kuhusika katika mauaji hayo

Show More

Related Articles