HabariMilele FmSwahili

Sarah Cohen na Peter Karanja kujibu mashtaka ya mauaji mahakamani leo

Mjane wa mfanyibiashara Tob Cohen, Sarah Cohen pamoja na mshukiwa mwenza Peter Karanja wanatarajiwa mahakamani leo kujibu mashtaka ya mauaji.

Hii ni baada ya mahakama kuagiza  Sarah Cohen kufanyiwa uchunguzi wa kiakili wiki jana. Bi Cohen pamoja na Karanja wamekuwa korokoroni kwa takribani majuma mawili baada ya kuhusishwa na kutoweka marehemu Cohen ambaye mwili wake ulipatikana wiki jana katika makazi yake mtaani Kitisuru hapa Nairobi. Familia ya Cohen ikiongozwa na dadake Gabrielle Van Straten imeelezea matumaini ya kupata haki mahakamani.

Hata hivyo washukiwa kupitia mawakili wao wamewasuta vikali polisi kwa namna wanavyoendesha uchunguzi kuhusiana na mauaji ya Cohen

Show More

Related Articles