HabariMilele FmSwahili

Safaricom yazindua nembo ya M-pesa kama heshima kwa Eliud Kipchoge

Kampuni ya Safaricom imezindua nembo ya M-Pesa itakayotumika siku saba zijazo kama heshima kwa mwanariadha Eliud Kipchoge.

Nembo hiyo mpya itakuwa na jina, Eliud na nambari 1:59 muda ambao Kipchoge anatarajiwa kuutumia kukimbia Jumamosi hii jijini Vienna, Austria.

Kaimu afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Safaricom Micheal Joseph amesema hatua hiyo ni ishara taifa linamuenzi Kipchoge kuwa mwanariadha aliye na kipaji ambacho kimeliweka taifa hili mbele kwenye riadha.

Show More

Related Articles