HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta awasili Eldoret kuongoza ufunguzi wa kiwanda cha Rivertex

Rais Uhuru Kenyatta awasili katika eneo la Kapsaret Eldoret kuongoza ufunguzi wa kiwanda cha pamba cha Rivertex. Ni ziara inayotarajiwa kushuhudia siasa. Hata hivyo baadhi ya wanasiasa wa eneo hilo wakiongozwa na mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi na Caleb Kositany wa Soi wamepuuzilia mbali kauli kuwa ujio wa rais utaibua hisia kali za kisiasa.

Wakati uo huo waziri wa viwanda Peter Munya amesema ufunguzi wa kiwanda cha Rivertex ni mwanzo wa azma ya serikali kuvikwamua viwanda nchini. Munya ambaye alifika mapemakatika kiwanda hicho amesema rais Kenyatta amejitolea kuhakikisha kuwa sekta ya utengezaji bidhaa ambayo ni moja wapo ya ajenda nne kuu za utawala wake imeirakika hata zaidi

Show More

Related Articles