HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta kufungua rasmi kongamano la COMESA kesho katika ukumbi wa KICC

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kufungua rasmi kongamano la siku tano la kibiashara la COMESA hapo kesho katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa KICC. Kongamano hilo litakalodumu hadi tarehe 21 mwezi huu wa Julai unatarajiwa kuwaleta pamoja wadau kutoka sekta ya umma na ya kibinafsi katika biashara kujadili jinsi ya kuboresha biashara katika muungano wa COMESA.

Baadaye wiki hii rais anatarajiwa kuzindua mradi wa uzalishaji kawi kupitia upepo huko Marsabit. Ni mradi unaotajika kuwa mkubwa wa aina yake barani Africa katika ziwa Turkana eneo la Loyangalani. Mradi huo unatarajiwa kuzalisha megawati  310.

Show More

Related Articles