HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta akutana na kufanya mashauriano wa mwenyeji wake Xi Jinping wa China

Rais Uhuru Kenyatta leo amekutana na kufanya mashauriano na rais wa China Xi Jinping Jijini Beijingi. Mkutano huo umeangazia uhusiano baina ya mataifa haya mawili huku Kenya ikitarajia kupokea mkopo wa shilingi bilioni 368 kufadhi ujenzi wa reli ya kisasa kutoka naivasha kuelekea kisumu. Rais Kenyatta pia anatarajiwa kuhudhuria kongamano la baraza la ushirikiano wa kimataifa la “Ukanda mmoja, njia moja. Akihutubu awali katika kongamano hilo mwakilishi wa Umoja wa Afrika kuhusu miundo msingi Raila Odinga ameyahimiza matiafa ya Afrika kuainisha miradi yao ya miundo msingi kuambatana na mahitaji ya kikanda. Raila anasema hatua hii imtaimarisha utangamano wa nchini za ukanda huu.

Show More

Related Articles