HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta afanya ziara ya ghafla katika kituo cha kuhifadhi makasha Embakasi

Rais Uhuru Kenyatta amefanya ziara ya ghafla katika kituo cha kuhifadhi makasha yanayosafirishwa na reli ya kisasa kutoka bandari ya Mombasa cha Embakasi. Ziara ya rais inafuatia lalama za wafanyibiashara kuhusiana na jinsi bidhaa zao zimekuwa zikinaswa na kuzuiliwa katika kituo hicho. Katika ziara hiyo ya kutathmini utendakazi katika kituo hiki rais Kenyatta ameandamana na waziri wa usalama wa kitaifa dkt Fred Matiangi na katibu wake Karanja Kibicho.

Show More

Related Articles