HabariMilele FmSwahili

Profesa Margret Kobia aunga mkono wafanyikazi wa umma kustaafu na miaka 60

Profesa Margret Kobia ameunga mkono wafanyikazi wa umma kustaafu na miaka 60. Kobia ambaye anahojiwa na bunge kubaini uwezo wake wa kuhudumu kama waziri wa utumishi wa umma,anasema umri huo ni sawa kwa mkenya yeyote kutekeleza majukumu yake bila changamoto. Kobi anasema kwa sasa ni asilimia 19 pekee ya vijana walio chini ya miaka 35 ambao wameajiriwa katika sekta ya utumishi wa umma. Aidha amewaeleza wabunge hao wakiongozwa na spika Justine Muturi kuwa hana doa katika utendakazi wake wabunge wanaoshiriki zoezi la ukaguzi wametaka kujua jinsi profesa Kobia atakabiliana na ufisadi hasa kwenye idara ya nys ilio chini ya wizara yake

Show More

Related Articles