HabariMilele FmSwahili

Polisi wanasa mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku yenye dhamani ya milioni 2 Eldoret

Watu watatu wamekamatwa kufuatia msako uliopelekea kunaswa shehena ya mifuko ya plastiki inayokisiwa kuwa ya dhamani wa shilingi milioni 2  mjini Eldoret. Maafisa wa mamlaka ya NEMA waliohusika katika msako huo wamedhibitisha kuwa mifuko hiyo imepatikana katika  jengo la mfanyibiashara mmoja mtaani Eastleigh jijini humo. Oparesheni  hiyo  imeendeshwa na kamati ya usamala kutoka eneo la Turbo kwa ushirikiano na idara tofauti za serikali ikiwamo ya mafisa wa idara ya mazingira NEMA. Hata hivyo mfanyibiashara huyo amekana kuuza mifuko hiyo.

Show More

Related Articles