HabariMilele FmSwahili

Polisi wamsaka kijakazi aliyewapa sumu watoto wa mwajiri wake na kusababisha kifo cha mmoja kaunti ya Migori

Polisi Kaunti ya Migori wanamsaka kijakazi aliyewapa sumu watoto 3 wa mwajiri wake na kijakazi aliyefika kuchukua nafasi yake katika mtaa wa Makaazi wa Oruba. Inaarifiwa mtoto mmoja amefariki kufuatia kisa hicho cha jana asubuhi huku ndugu zake wawili na kijakazi huyo wakiendelea kupokea matibabu katika hospitali ya kimisheni ya st. Joseph Ombo. Mamake watoto hao kwa jina Bertha Oluoch anasema kijakazi huyo aliwapakulia chakula hicho cha jio wanawe wanne japo wawili walifeli kukila. Sasa polisi wanatoa wito kwa yeyote aliye na taarifa kuhusu aliko kijakazi huyo kushirikiana na polisi ili kuhakikisha mshukiwa anakamatwa

Show More

Related Articles