HabariMilele FmSwahili

Polisi Trans Nzoia wamsaka mama anayedaiwa kumuua mwanawe wa mwaka 1

Polisi katika kaunti ya Trans Nzoia wanamsaka mama anayedaiwa kumuua mwanawe wa mwaka mmoja katika kijiji cha Khalwenge eneo bunge la  Endebess. Inadaiwa mama huyo alitoroka baada ya kumuua mtoto huyo na kuutupa mwili wake katika shimo usiku wa kuamkia leo . Babake mtoto Jeremiah Wafula anasema hakukuwa na mzozo baina yake na mama huyo.

Show More

Related Articles