HabariMilele FmSwahili

Polisi Kitui wamsaka mzee 1 kumnajisi msichana wa miaka 14

Polisi eneo la Mwingi ya kati kaunti ya Kitui wanasaka mzee mwenye umri wa miaka 60 aliyenajisi mshichana mwenye umri wa miaka 14 katika kijiji cha Thitha eneo ilo la Mwingi ya kati kaunti ya Kitui jana jioni. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa utawala John Gitaru Githae msichana aliyenajisiwa anapokea matibabu katika hospitali ya Mwingi Level 4 kaunti ya Kitui huku akiwataka wananchi kusaidia kumnasa mshukiwa hiuyo kwa kutoa ripoti kwa polisi.Visa vya ubakaji na unajisi wa watoto wenye umri mdogo pamoja na ulawiti wa watoto wa kiume vimekuwa vikuchipuka mara kwa mara kwenye eneo la Mwingi kaunti ya Kitui, jambo lililomchangia mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kitui Irene Kasalu kupendekeza wote wanaopatikana wakitekeleza uovu huo kuadhibiwa vikali.

Show More

Related Articles