HabariMilele FmSwahili

Polisi bandia akamatwa mjini Migori

Polisi mjini Migori wamemkamata jamaa mmoja wa  umri wa makamo ambaye ni polisi bandia. Kwa mujibu wa kamanda Joseph Nthenge, mshukiwa Anthony Obare alikuwa akiwahangaisha manesi katika hospitali ya rufaa ya kaunti hiyo kabla yao kupiga ripoti kwa polisi alipokamatwa. Mshukiwa huyo anayetarajiwa kufikishwa mahakamani leo amepatikana na kitambulisho ghushi cha polisi, Kamanda Nthenge akiahidi uchunguzi wa kina kuwatia mbaroni washukiwa wengine.

Show More

Related Articles