HabariMilele FmSwahili

ODM yajitenga na madai ya kuidhinisha hoja ya kubanduliwa afisini kwa Onyango Oloo

Chama cha ODM  kimejitenga na madai ya kuidhinisha hoja ya kumbandua afisini spika mwenye utata Onyango Oloo.

Kupitia taarifa mwenyekiti wa ODM John Mbadi anasema hakuna mkutano wowote wa kitaifa ulioandaliwa kuidhinisha hatua hiyo.Ni taarifa inayojiri usalama ukiimarishwa ndani na nje ya bunge la Kisumu baada ya kushuhudiwa vurugu kumzuia Oloo kuingia katika bunge hilo

Hata hivyo Oloo anashikilia ni yeye ndiye spika wa bunge hilo na kudai uteuzi wa Elisha Oraro kama kaimu spika ni kinyume na sheria.

Oloo aliyeachiliwa kwa dhamana ya shilingi anakabiliwa  na mashtaka ya ufujaji wa zaidi ya shilingi bilioni 2 katika hazina ya maendeleo ya Lake Basin.

Show More

Related Articles