HabariMilele FmSwahili

Ni hatia mbwa wako kubweka ka dakika sita mfululizo na utapigwa faini ya shilingi 5000

Wanaofuga mbwa hapa Nairobi sasa huenda wakalazimika kuwasafirisha kwingine au kuwacha kuwafuga.Hii ni kufuatia sheria mpya ambayo inapinga mbwa wako kubweka kwa muda wa dakika sita mfululizo kwa saa moja au dakika tatu mfululizo kwa muda wa dakika thelathini.Kulingana na sheria hiyo, utapigwa faini ya shilingi 5000 au kifungo cha miezi miwili endapo mbwa wako atapatikana akikiuka sheria hii.Hata hivyo kulingana na wataalam ni vigumu kumfunza mbwa jinsi ya kubweka na kukimya baada ya wakati fulani.Pia wamiliki mbwa wanahisi kuwa sheria hii haina mashiko yoyote kwani hakuna mbinu itakuwa vigumu kutoa ushahidi kortini. Sheria hiyo pia inataka mbwa aliye na umri wa miezi sita kuwa na leseni na kitambulisho kutoka kwa kaunti ya Nairobi.Kukosa kufanya hilo utatozwa faini kati ya shilingi 2000 na 5000 ili kurejeshwa mbwa wako”

Show More

Related Articles